Geuza Zawadi yako kuwa Msaada kwa Mtoto wa Mtaani
Unasherehekea siku yako ya kuzaliwa hivi karibuni na hujui ni zawadi gani unahitaji kwa vile una kila kitu tayari? Au unakaribia kuacha kazi au kustaafu na watu wanakuuliza unahitaji zawadi ya aina gani? Au kuna matukio mengine ambapo zawadi hutolewa? Omba zawadi kwa ajili ya mtoto wa mtaani, Mwanza Tanzania. Watoto wa Upendo Daimwa watafaidika nayo sana.
-
Kiasi cha €25 kinanunua vitabu vitatu vya kujifunza na kujisomea kwa ajili ya kituo cha elimu ambapo watoto hupata masomo ya ziada.
-
Kiasi cha €35 kinanunua sare 5 kwa ajili ya kikundi chetu cha sarakasi kinachofanya maonyesho kadhaa mahotelini ili kukusanya kipato.
-
Kiasi cha €40 kinasaidia kwa mwezi mzima mtoto mmoja wa mitaani wa Upendo Daima. Kitamsaidia mtoto kwenda shule, kununulia chakula na maji, kupata malezi, mavazi na malazi.
-
Kiasi cha €50 kinachangia ununuaji wa vifaa vya kuzalishia umeme wa mionzi ya jua.
-
Kiasi cha €60 kinagharamia huduma za afya kwa watoto 5 kwa mwezi mzima.
-
Kiasi cha €75 kinanunua vyandarua vitano.
- Kiasi cha €100 kinaisaidia timu yetu kufanya kazi kwa wiki mbili ya kuwasaidia watoto kuachana na maisha ya mtaani.
Tazama tafadhali kwenye duka letu kupitia sehemu ya juu kulia kwenye mtandao.