Upendo Daima - Mradi wa Watoto wa Mitaani Tanzania

["\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_1_20130225_1380602795.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_2_20130225_1915094524.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_3_20130225_1269161720.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_4_20130225_1203900127.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_5_20130225_1696649307.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_6_20130225_1470469504.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_7_20130225_1778566945.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_8_20130225_1522298131.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_9_20130225_1837204428.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_10_20130225_1305918366.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_11_20130225_1235579240.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_12_20130225_1103703416.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_13_20130225_1614865694.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_14_20130225_1269038727.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_15_20130225_1817561193.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_16_20130225_1232435165.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_17_20130225_1134651688.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/teambuilding2_1_20180221_1520592193.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/teambuilding_1_20180221_2070968253.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/homevisit_1_20180221_1377088869.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/homevisit_2_20180221_1506278386.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/homevisit_3_20180221_1738804695.jpg"]

Wafadhili wa Kitanzania

Kwa sasa tunajitahidi kupata wafadhili zaidi kutoka Tanzania. Lengo letu ni kutokuwa tegemezi kwa misaada ya kimataifa, kwani suala la kulea watoto wa mitaani linatakiwa kufanywa na nchi yenyewe. Kumekuwa na ongezeko la misaada ya watu hapa, hasa misaada katika vitu.

arusha2Arusha 1

Kati ya Septemba na Oktoba mwaka huu, makundi matatu yalitembelea Malimbe. Kwanza tulitembelewa na wakimbiaji 21 kutoka Team Fitness, Arusha waliokuwa wamekimbia mbio za masafa ya kati. Kikundi chetu cha sarakasi na ngoma kilifanya onyesho zuri sana. Wageni walifurahia sana na pia walifurahi kuona na kusikia juu ya kazi zetu. Walijionea Back Home House ambapo tunawaandaa watoto kuwezi kurudi kwenye familia zao. Walileta mchele, mikate, mafuta ya kupikia, chai na fedha nyingi. Kiongozi wa kikundi alizungumza na watoto, akawaasa kujituma ili kujenga maisha bora zaidi japokuwa walianza na maisha magumu mtaani.

lions1lions3lions 4

Wiki hiyo hiyo Lions Club ya Mwanza ilitutembelea. Tuliwaelezea juu ya kazi tunazozifanya; tuliwaonyesha mazingira na kuwaburudisha kwa sarakasi na ngoma. Ili kuweka kumbukumbu, mmea wa bilingani ulipandwa katikati ya bustani yetu kama ishara ya urafiki. Lions Club walileta zawadi mbalimbali kama vile vitabu, kalamu, unga, maziwa, juisi za matunda, biskuti  na maandazi. Katika hotuba yao, waliwasifia wafanya kazi kwa kazi kubwa ya kijamii wanayoifanya mkoani Mwanza.

crbd1crbd 2crbd4crbd5

Tarehe 8 Oktoba, tulitembelewa na benki ya CRDB ikiwa ni sehemu yao ya kufanya shughuli za kijamii. Walikaribishwa na kupewa maelezo juu ya kazi zetu na kisha walipata burudani mbalimbali za michezo kutoka kwa watoto. Inafurahisha sana kuona namna watoto wanavyomudu michezo hii na pia inavyoburudisha kila mara inapofanyika. Wafanyakazi wa benki walifika na zawadi mbalimbali pia. Walileta sukari, mafuta ya kupikia, mahindi na mchele, vitabu na kalamu.

Ziara hizi ni faraja kubwa kwetu, si kwa sababu ya zawadi tu, bali pia zinaonyesha hatuko peke yetu na kwamba kazi hii inakubalika katika jamii inayotuzunguka.

Habari za Hivi Karibuni

  • March 2019 Twee weken lang acties voor Upendo Daima bij Montessori school Tuinstad Schiebroek te Rotterdam. De tienjarige Ruben en zijn vrienden voelen zich nauw betrokken bij het wel e...
  • Januari 5, 2018 wafanyakazi wa UD walikwenda kwa hafla ya mapumziko na kuimarisha ushirikiano katika mwambao wa ziwa Victoria Mwanza panaitwa Avashi, yapata km 5 kutoka Malimbe Family. Lengo ...
  • Asanteni sanaMatokeo ya pili ya wafadhili wa riadha yaliyoandaliwa na wanafunzi kutoka katika shule ya Lise Meitner huko Moordeich Ujerumani yalizidi matarajio yaliyotegemewa:Wanafunzi 367 wa daras...
  • Octoba 28, 2017 Jina langu ni Mara le Mahieu Miaka minne iliyopita nilijiunga na Upendo Daima kama Mlei wa Misionari kutoka SMA. Ilikuwa fursa nzuri sana kwangu ya kufanya kazi na...

Back Home House

Malimbe Family