Watoto wa mtaani mjini Mwanza
Watoto wanaishia mtaani kwa sababu ya kutelekezwa au kufiwa na wazazi wao. pia wanashinda njiani kwa sababu ya hali ya umaskini nyumbani kwao. Mara kwa mara familia wanatembeza watoto wao mtaani ili waende kupata hela.
Mtaa ni nyumbani kwao na wakati mwingine wanawaona watoto wenzao wa mtaani kama familia zao. Watoto wanajipanga katika vikundi ili watafute maisha. wanajaribu kupata kazi ndogo ndogo au wanaibaiba. Wamezoea kupigana na kuombaomba kwa ajili ya chakula. Biashara ya madawa ya kulevya ni kawaida kwao.
Wanalala mtaani bila ya kulindwa na mara kwa mara wanafukuzwa na polisi. Watoto wa mtaani wengi wanakabili vitendo vya vurugu na makosa ya kinyumba. Ni rahisi kwao kuambukizwa na ukimwi au maradhi mengine ya kueneza kwa kujamiiana. Ikiwa ni wagonjwa hawana fedha ya kwenda kwa daktari au ya kupata matibabu. Mara nyingi hawajiheshimu hata kidogo.
Kutokana na hali hiyo ya taabu watoto wa mtaani wengi wananusanusa gundi au tina za rangi. Kitambo kidogo hawaoni njaa wala baridi na maumivu yanapunguka. Hata hivyo kunusanusa huko kunaathiri ubongo wao na mwishowe hali yao inazidi kuwa mbaya.