Upendo Daima - Mradi wa Watoto wa Mitaani Tanzania

["\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_1_20130225_1380602795.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_2_20130225_1915094524.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_3_20130225_1269161720.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_4_20130225_1203900127.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_5_20130225_1696649307.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_6_20130225_1470469504.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_7_20130225_1778566945.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_8_20130225_1522298131.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_9_20130225_1837204428.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_10_20130225_1305918366.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_11_20130225_1235579240.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_12_20130225_1103703416.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_13_20130225_1614865694.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_14_20130225_1269038727.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_15_20130225_1817561193.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_16_20130225_1232435165.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_17_20130225_1134651688.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/teambuilding2_1_20180221_1520592193.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/teambuilding_1_20180221_2070968253.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/homevisit_1_20180221_1377088869.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/homevisit_2_20180221_1506278386.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/homevisit_3_20180221_1738804695.jpg"]

Ziara/Likizo

Mwezi 6,  2016

Ili kupata uelewo mzuri wa kazi zetu, nilikwenda kutembelea moja ya familia za watoto wetu. Likizo imeanza sasa na niliweza kusafiri na Mama Lucy aliyekuwa akimpeleka mtoto, Juma Kurwa nyumbani kwa ajili ya mapumziko.

Ziara hii ilikuwa maalum, kwa vile ilikuwa mara yake ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu kuonana na familia yake. Juma aliishi Mwaza mama yake alipofariki na baba yake kuwa mgonjwa sana. Alianza kuishi mitaani na baadaye aliletwa Malimbe Family. Ilishindikana kumuunganisha tena baba yake ambaye alikuwa amekataliwa na familia yake kwa sababu za ugonjwa wake. Upendo Daima imejitahidi kuwa na mawasiliano na baba yake mpaka alipotoweka ghafla. Baadaye kupitia watu wengine Upendo Daima walipata mawasiliano naye tena na kujua kuwa alirudi nyumbani Bukoba na kwamba afya yake ilikuwa na unafuu sasa. Baba Juma pamoja na familia yake walikubali kumpokea Juma kwa ajili ya likizo.

Baada ya ziara hii, nimezidi kuwaheshimu watoa ushauri nasaha ambao hufanya ziara za namna hii mara kwa mara.

Safari yetu ilianza saa kumi na mbili alfajiri kwa basi liendalo Bukoba. Baada ya masaa saba tulifika Muleba na kubadili usafiri kwa kupanda daladala. Tulisafiri milimani na baada ya nusu saa tulifika kwenye kijiji ambapo tulibadili usafiri tena. Tuliwasili kwenye kijiji ambacho ndugu wa Juma walidhaniwa kuishi. Tuliuliza wazee wa kijiji na kuita watu kadha wa kadha ambao walitusaidia kusafiri kwa pikipiki  kuelekea familia ya Juma. Safari hii ilichukua dakika 20 kupitia njia ndogo kwenye mashamba ya migomba.

huisbezoek/ bus

 huisbezoek bus 2 huisbezoek bus3

Familia ya Juma ilifurahi mno kumuona. Tulikutana na baba yake, mjomba, kaka, babu na bibi, shangazi, shemeji na watoto wengi. Tulikaribishwa vizuri sana na kuonyeshwa mashamba, nyumba na pia tulipewa chakula na kuwa na mazungumzo mazuri sana. Tulijisikia vizuri kumuacha Juma nyumbani kwa ajili ya likizo.

Kutoka pale tuelekea Bukoba. Familia ilitushauri kuwa hakuna haja ya kuchukua pikipiki, tungeweza kutemebea kwa miguu mpaka barabara kuu. Tulianza kutembea saa kumi na moja jioni, baada ya dakika 20 tulikuwa bado hatujafika kwenye barabara, na tulipoona pikipiki tuliichukua hiyo. Safari ilichukua dakika 15 na tuliweza kupata daladala kwenye kijiji kilichofuata. Gari hili lilikuwa likielekea Bukoba, lakini baada ya dakika 20 dereva alisimama kijijini na kutueleza kuwa huu ndio ulikuwa mwisho wa safari yake. Tulitafuta pikipiki tena na tuliweza kuendelea na safari kwenye barabara ya vumbi kwa dakika 20 tulipoifikia barabara kuu. Hapa tulilazimika kubadili usafiri tena na kuchukua daladala iliyotufikisha Bukoba.

Pamoja na yote, tulikuwa na bahati sana kwani mara nyingi hutokea pia kuwa baada ya safari yote hii unaweza usiipate familia, au ukakuta walishahama, n.k.

Ninapenda kutoa heshima yangu kubwa kwa wafanyakazi wanaofanya safari hizi mara nyingi. Kwangu mimi safari moja ilitosha kabisa.

 

Habari za Hivi Karibuni

  • March 2019 Twee weken lang acties voor Upendo Daima bij Montessori school Tuinstad Schiebroek te Rotterdam. De tienjarige Ruben en zijn vrienden voelen zich nauw betrokken bij het wel e...
  • Januari 5, 2018 wafanyakazi wa UD walikwenda kwa hafla ya mapumziko na kuimarisha ushirikiano katika mwambao wa ziwa Victoria Mwanza panaitwa Avashi, yapata km 5 kutoka Malimbe Family. Lengo ...
  • Asanteni sanaMatokeo ya pili ya wafadhili wa riadha yaliyoandaliwa na wanafunzi kutoka katika shule ya Lise Meitner huko Moordeich Ujerumani yalizidi matarajio yaliyotegemewa:Wanafunzi 367 wa daras...
  • Octoba 28, 2017 Jina langu ni Mara le Mahieu Miaka minne iliyopita nilijiunga na Upendo Daima kama Mlei wa Misionari kutoka SMA. Ilikuwa fursa nzuri sana kwangu ya kufanya kazi na...

Back Home House

Malimbe Family