Upendo Daima - Mradi wa Watoto wa Mitaani Tanzania

["\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_1_20130225_1380602795.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_2_20130225_1915094524.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_3_20130225_1269161720.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_4_20130225_1203900127.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_5_20130225_1696649307.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_6_20130225_1470469504.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_7_20130225_1778566945.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_8_20130225_1522298131.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_9_20130225_1837204428.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_10_20130225_1305918366.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_11_20130225_1235579240.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_12_20130225_1103703416.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_13_20130225_1614865694.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_14_20130225_1269038727.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_15_20130225_1817561193.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_16_20130225_1232435165.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/slideshow_17_20130225_1134651688.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/teambuilding2_1_20180221_1520592193.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/teambuilding_1_20180221_2070968253.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/homevisit_1_20180221_1377088869.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/homevisit_2_20180221_1506278386.jpg","\/images\/joomgallery\/details\/slideshow_2\/homevisit_3_20180221_1738804695.jpg"]

Malimbe Family

Malimbe Family
Sehemu ya zamani ya kupigia kambi.
Katika kijiji cha Malimbe, kama 10 km kusini mwa jiji la Mwanza kuna sehemu ya zamani ya kupiga kambi. Lina ukubwa wa  ekari 4 na liko katika ardhi yenye miamba, si mbali kutoka Ziwa Victoria. Mama Marga, kana kwamba naitwa na watoto, aliona sehemu hii kama peponi kwa watoto wa mitaani wakati akinunua eneo hili mwaka 2003. Leo eneo hili lina mabweni kadhaa ya Kiafrika, ofisi na nafasi ya kuhifadhia vitu, vibanda viwili, kituo cha kujifunza na nafasi ya ofisi na maktaba (iliyojengwa mwaka 2012). Kuna pia uwanja mdogo wa mpira na shamba (bustani ya mboga). Eneo lote limezungukwa na uoto wa asili mzuri na miembe na mimea aina ya bougainvillea. Hoja Tarsisius ni meneja wa kituo hiki cha Malimbe Family. Hoja na timu yake wamefanya kazi kubwa ya kutengeneza eneo hili kuwa zuri na pia kuzifanya nyumba zikalike. Kuna taa katika kila nyumba (kwa kutumia nishati ya jua ) na kuna maji ya bomba. Majani kwa ajili ya kuzibia paa za nyumba yameandaliwa. Maeneo ya kufanyia usafi, vyoo, matenki ya maji na maeneo ambapo watoto wanaweza kufua nguo yamejengwa.

Tanzania MF

 

 

 

 

Watoto
Kwa wastani wavulana 50 wenye umri wa miaka kati ya 8 na 18 huishi pamoja kama familia moja kubwa ya Afrika chini ya uongozi wa wa Upendo Daima. Watoto ambao hukaa katika Malimbe Family hawawezi (kwa wakati huu) kurudi nyumbani.
Timu imepata mafunzo juu kuelimisha, kuongoza na kutoa ushauri nasaha kwa watoto.
Kila asubuhi watoto wanakwenda shule ya msingi na timu inawasiliana mara kwa mara na walimu. Baada ya kuja nyumbani kutoka shule chakula huwa kimeandaliwa tayari kwa ajili yao. Chakula hupikwa na matron ambaye pia ni muuguzi. Wakati wa mchana watoto kufanya kazi zao za nyumbani na kupata masomo ya ziada katika kituo cha kujifunzia. Watoto wanaoishi kwenye vijiji jirani wanaweza pia kuhudhuria masomo haya. Baada ya hapo kuna wakati wa kucheza mpira wa miguu. Kila jioni "babu"  hukaa pamoja na watoto wakiota moto. Babu huwasimulia hadithi za jadi, zinazoelimisha  na baadaye watoto wanaweza kujieleza kwa urahisi zaidi na kujadiliana juu ya matatizo yanayowakumba.

Shamba
Katika eneo hili pia kuna shamba (bustani ya mboga) na kuna mbwa kadhaa. Watoto hujifunza bustanini namna ya kupanda na kutunza mboga. Wanapanda mahindi, mchicha, nyanya na karanga. Watoto hujifunza jinsi ya kutunza wanyama na bustani na kwa njia hii hujifunza kuchukua majukumu ya wenyewe juu ya mahitaji yao ya kila siku kama ilivyo desturi nchini Tanzania.

Warsha
Mbali na timu ya kudumu, kuna watu wengine pia ambao mara nyingi hujitolea  kuandaa warsha na matamasha maalumu. Hii ni kwa njia ya michezo na maigizo. Kupitia maigizo na kujieleza watoto hujifunza tofauti kati ya mema na mabaya. Uelimishaji unakwenda kwa njia ya maigizo na michezo. Muziki, ngoma na sarakasi huwapa watoto uwezo wa kujieleza na kwa kufanya hivyo kurejesha heshima yao.

Habari za Hivi Karibuni

  • March 2019 Twee weken lang acties voor Upendo Daima bij Montessori school Tuinstad Schiebroek te Rotterdam. De tienjarige Ruben en zijn vrienden voelen zich nauw betrokken bij het wel e...
  • Januari 5, 2018 wafanyakazi wa UD walikwenda kwa hafla ya mapumziko na kuimarisha ushirikiano katika mwambao wa ziwa Victoria Mwanza panaitwa Avashi, yapata km 5 kutoka Malimbe Family. Lengo ...
  • Asanteni sanaMatokeo ya pili ya wafadhili wa riadha yaliyoandaliwa na wanafunzi kutoka katika shule ya Lise Meitner huko Moordeich Ujerumani yalizidi matarajio yaliyotegemewa:Wanafunzi 367 wa daras...
  • Octoba 28, 2017 Jina langu ni Mara le Mahieu Miaka minne iliyopita nilijiunga na Upendo Daima kama Mlei wa Misionari kutoka SMA. Ilikuwa fursa nzuri sana kwangu ya kufanya kazi na...

Back Home House

Malimbe Family