Kujitolea
Unakaribishwa kujitolea. Kwanza kabisa kwa kusaidia shughuli hapa Uholanzi. Pia kuna fursa ya kufanya kazi za kujitolea nchini Tanzania. Ukipenda kwenda Tanzania tunahitaji kulishughulikia suala hili kwa makini sana. Lugha na mazingira ya kazi ni tofauti sana na bila kuwa na uzoefu na uelewo wa kazi katika nchi zinazoendelea, anayejitolea huwa mzigo wa ziada kwenye timu. Kama unafikiri kwamba kweli unaweza kuongeza thamani na unapatikana kwa angalau nusu mwaka au zaidi na kuwa unaielewa kidogo lugha ya Kiswahili, tafadhali wasiliana na Marga van Barschot (Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona. )